
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Rais wa Zambia Hakainde Hichilema
Kauli hiyo ameitoa hii leo Agosti 2, 2022, jijini Dar es Salaam, mara baada ya kumaliza mazungumzo ya faragha na mgeni wake Rais wa Zambia Hakainde Hichilema, Ikulu ya Dar es Salaam.
"Tumekubaliana na ndugu yangu Hichilema kwamba turudi turudishe ule undugu kama tulivyoachwa na wazazi wetu, tumeangalia uhusiano wa kisiasa nchi zetu kwa yoyote yaliyotokea lakini lazima turudi sisi kama viongozi wa nchi tuwaongoze watu wetu waelewane vizuri," amesema Rais Samia
Tazama video hapa chini