Monday , 15th Aug , 2022

Mgombea Urais kupitia chama cha UDA nchini Kenya William Ruto, ametangazwa kuwa mshindi wa kiti hicho hii leo.

William Ruto, Mteule Urais nchini Kenya

Matokeo hayo yametangazwa hii leo Agosti 15, 2022, na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini Kenya (IEBC), Wafula Chebukati, na kusema Ruto amepata zaidi ya kura milioni 7 akifuatiwa na mshindani wake Raila Odinga, aliyepata zaidi ya kura milioni 6.

Matokeo ya Urais nchini Kenya yametangazwa wakati ambao, Tume ya IEBC ikiwa imegawanyika kwa baadhi ya maafisa wa tume hiyo.