Monday , 22nd Aug , 2022

Mahakama ya wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza imewahukumu kifungo cha Maisha jela watu wawili kwa kosa la kulawiti Watoto wenye umri wa miaka mitano na miaka 10

Kati ya waliohukumiwa kifungo hicho ni kijana mwenye umri wa miaka 28 aitwaye Juma Omary mkazi wa Mkuyuni jijini Mwanza ambae ni fundi ujenzi, inadaiwa mwaka jana alimdanganya mtoto wa Jirani yake mwenye umri miaka mitano kuwa atampa kitu kizuri ndipo akampeleka kichakakani na kumlawiti

Mtuhumiwa huyo alipopewa nafasi ya kujitetea alisema siku ya tukio alikuwa amelewa na hakutenda kosa hilo, huku hakimu mkazi wa mahakama ya wilaya ya Nyamagana Sheila Manento akisema kifungo hicho kiwe fundisho kwa wengine watakajaribu kufanya kitendo kama hicho

Katika kesi nyingine namba 49 ya kulawiti mwanaume aitwaye Ismail Abeid Bulashi mwenye umri wa miaka 35 mkazi wa mtaa wa Nyerere B kata ya Mabatini Mwanza, nae amehukumiwa Kwenda jela Maisha kwa kumlawiti mtoto mwenye umri wa miaka kumi

Ismail ambae ni mfanyabiashara mdogo anayeuza bidhaa mbalimbali zikiwemo na pipi inadaiwa mwezi wa tatu mwaka huu alimdanganya mtoto huyo kwa kumpa pipi ndipo akamlawiti

Akitoa hukumu ya kesi hiyo hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Nyamagana Veronica Mugendi amesema mtuhumiwa huyo ametenda kosa hilo kinyume na kifungu 154 kifungu kidogo na cha sheria ya kanunni ya adhabu sura namba 16 ya mwaka 2019