Wednesday , 24th Aug , 2022

Jeshi la Polisi mkoani Mbeya, limemkamata Mukhsin Mgaza mwenye umri wa miaka 24 ambaye ni dereva wa Lori lililosababisha ajali baada ya gari kufeli breki na kugonga mengine manne na kusababisha vifo vya watu 19 na majeruhi 31 eneo la mteremko wa Inyala Pipeline mkoani Mbeya Agosti 16, 2022

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei amesema baada ya dereva huyo kusababisha ajali alikimbia ndipo Jeshi la Polisi lilianza msako na kufanikiwa kumkatama

Katika hatua nyingine Jeshi la Polisi mkoani Mbeya limethibitisha kumshikilia  Karani mmoja wa sensa ya watu na makazi aliyelipwa  fedha za ushiriki wa zoezi hilo lakini hakushiriki