
Mtoto aliyeshughudia tukio hilo akisimulia
Shuhuda wa tukio hilo anasema kipindi anampiga kosa lilikuwa ni kushika Kanzu yake ambapo alimvuta na kumpiga ngumi ya kwenye mbavu
Baada ya tukio hilo mtoto huyo alilia na kwenda kumwambia mama yake kuwa ana maumivu kwenye ubavu ambapo mama yake alimwambia akamwambia kuwa kesho yake ndio angempeleka hospitali
Inaelezwa kuwa baada ya baada ya kufanya vipimo vyote waligundua kwamba bandama imejeruhika na damu inavujia ndani ya tumbo
Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Geita Ally Kitumbu amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo mtuhumiwa bado anashikiliwa kwa ajili ya uchunguzi