Sunday , 4th Sep , 2022

Mkuu wa wilaya ya Kigoma Ester Mahawe, amewahimiza wasomi na wakuu wa idara mbalimbali mkoani humo, kuanza kuzitumikia taaluma zao ili kuleta mabadiliko chanya kwa wananchi.

Mkuu wa wilaya ya Kigoma Ester Mahawe

Hayo ameyasema baada ya kubainika kuwa baadhi ya wasomi na watu wenye taaluma mbalimbali mkoani Kigoma kutoitumikia jamii kupitia elimu zao na kutajwa kuwa ndiyo sababu inayochangia kuendelea kuwepo kwa umaskini katika jamii hiyo.

Wakizungumza na Kurasa baadhi ya wakazi wa Halmshauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji, wamesema hali hiyo ni kutokana na baadhi yao kukosa uzalendo hali inayowapelekea kufanya kazi kwa maslahi yao binafsi.