Monday , 5th Sep , 2022

Umoja wa madalali zaidi ya 30 wa Kata ya Iwungilo, Halmashauri ya Mji Njombe, wameamua kuchangia ujenzi wa kituo cha afya ambacho kinatarajia kuanza ujenzi wake mapema mwezi huu ili kuwanusuru wananachi ambao mpaka sasa wanafuata huduma umbali mrefu.

Mdalali wa Kata ya Iwungilo

Madalali hao ni wanunuzi wa mazao mbalimbali katika eneo hilo na kwamba kila mmoja ametoa mchango wa shilingi laki moja.

Kwa kutambua umuhimu wa kituo hicho imeelezwa kwamba, Halmashauri ya Mji Njombe tayari imetenga kiasi cha shilingi milioni 250 ili kuongeza nguvu ya kukamilika kwa ujenzi huo.