Monday , 5th Sep , 2022

Wavuvi kanda ya ziwa wamemwangukia Makamu mwenyekiti wa CCM bara Abrahman Kinana na kumuomba kufikisha kilio chao kwa Rais kuhusu tatizo la uvuvi haramu na kuomba kulipwa fidia kutokana na oparesheni sangara ya mwaka 2018 iliyofanywa dhidi yao ambayo ilileta hasara ya fedha nyingi.

Wavuvi

Wakizungumza na waandishi wa Habari baada ya kutoka kwenye kikao cha ndani na Makamu Mwenyekiti Kinana wamesema toka mwaka 2018 hadi leo hii wavuvi wamekuwa na Maisha magumu kutokana na oparesheni hiyo, na kumuomb afikishe kilio chao kwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ili waweze kupewa fidia

"kulipita oparesheni tokomoeza mwaka 2018 lakini oparesheni hiyo ilikuwa na lengo la kuwatokomeza wavuvi wasiendelee na wawe masikini haikuwa na usimamizi mzuri na imezalisha hali ya umasikini na kuleta uvuvi haramu"- amesema Hassan Mhenga, Mvuvi

Licha ya Kinana kusema amezivchukua changamoto zao na atazifikisha sehemu husika mwenyekiti wa chama cha wavuvi nchini TAFU Bakari Kadabi akaeleza matarajio yao baada ya kikao hicho.