
kikosi cha Namungo FC.
Wakati wa maboresho hayo Namungo FC ilikuwa inatumia Uwanja wa Ilulu, Lindi na ulipofungiwa ili ufanyiwe maboresho walikuwa wanatumia Uwanja wa Mkapa na Uhuru kwa mechi za nyumbani.
Mazoezi yao ya kwanza ilikuwa ni Septemba 7,2022 na mashabiki wengi walijitokeza kushuhudia timu hiyo ikifanya mazoezi kwenye uwanja wao ambao kwa sasa una muonekano bora na wa kisasa zaidi.
Kinara wa utupiaji mabao ndani ya Namungo, Relliats Lusajo amesema kuwa kurejea kwao ni furaha na wataendelea kupambana kufanya vizuri.
“Tulikuwa nje kwa muda mrefu na tulikuwa tukitumia Uwanja wa Ilulu sasa tumerudi Uwanja wa Majaliwa hili ni jambo la kubwa kwetu.