Tuesday , 20th Sep , 2022

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi(CCM) Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein,leo ameongoza kikao Maalum cha kamati maalum ya halmashauri kuu ya CCM Taifa Zanzibar.

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi(CCM) Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein, na viongozi wengine wa CCM Zanzibar

Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa mikutano wa afisi kuu ya CCM,Kisiwandui Zanzibar ambapo pia kimepokea na kujadili kwa kina Taarifa ya kazi za Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya kwa kipindi cha miaka mitano 2017/2022.

Pamoja na hayo viongozi mbalimbali walioudhuria kikao hicho ni pamoja mjumbe wa kamati kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi,mjumbe wa kamati kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla.

Wengine ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Spika wa baraza la wawakilishi Zanzibar Mhe.Zubeil Ali Maulid pamoja na wajumbe wengine wa kamati kuu ya CCM Taifa na halmashauri kuu ya CCM Taifa Zanzibar.