Wednesday , 28th Sep , 2022

Wananchi na viongozi wa vijiji mbalimbali mkoani Mara wameliomba Jeshi la Polisi kuendelea na msako wa kuwakamata watu wanaojihusisha na vitendo vya ujambazi wa kutumia silaha vilivyoibuka mkoani humo hivi karibuni 

Mwenyekiti wa kijiji cha Nyamakobito wilaya ya Serengeti mkoani Mara, Mugale Chacha

Aidha wananchi hao wamelipongeza Jeshi la Polisi kwa kudhibiti vikali vitendo vya ujambazi katika maeneo yao
Kiongozi wa vikundi vya ulinzi wa jadi mkoani humo almaarufu kama 'Litongo Yusuph Wambura amesema vitendo vya ujambazi vimekuwa vikisababisha wananchi kuishi kwa hofu 

"Wananchi wanaishi kwa hofu, wafanyabiashara wanafilisiwa mali zao, wanavunja majumba ya watu usiku na kukosesha watu amani wakiwa na silaha, na wengine tunaishi nao na tunawafahamu hivyo tunashukuru Jeshi la Polisi kwa kupambana nao" - Amesema Yusuph Wambura 

Naye Mwenyekiti wa kijiji cha Nyamakobito wilaya ya Serengeti mkoani Mara, Mugale Chacha, ambae ni ndugu na jambazi aliyepoteza maisha katika tukio la mapambano ya kurushiana risasi na askari polisi hivi karibuni amelitaka Jeshi la Polisi nchini kuzidisha ulinzi na kuchukua taarifa za viongozi wa vijiji kwani ndugu yao huyo ameshajadiliwa sana katika vikao vya kiukoo ili kumdhibiti na tabia ya ujambazi wa kutumia silaha bila kukoma.

"Ndugu yangu Mugale ambae amepoteza maisha kwa vitendo vya ujambazi tulishamuasa sana aachane na vitendo hivyo, lakini mpaka mauti yanamkuta ni kweli jamii ilishamchoka, walishafungwa gereza la Butimba na taarifa zao zipo, vifungo kadhaa ila bado wanatoka wanarudi uraiani, hivyo sisi Mugale tulishamchoka kwa historia na vitendo vyake vya uhalifu na alikuwa anamiliki silaha za moto za kufanyia uhalifu".

Wananchi hao wamelitaka Jeshi la Polisi kuendelea na msako wa majambazi hao
Wananchi hao wanasema vitendo vya uhalifu wa silaha za moto ambavyo hutekelezwa na baadhi ya ndugu na wanafamilia wenzao katika kaya mbalimbali vinaathiri biashara na kufilisi mali za wakaazi wa mkoani huo