Rais wa Uganda Yoweri Museveni
Aidha katika barua yake aliyoiandika hii leo Oktoba 5, 2022, Rais Museveni pia, amewaomba msamaha wanajumuiya wa Afrika Mashariki pamoja na raia wa Uganda ambao walikerwa na maandiko ya Jenerali Kainerugaba kupitia ukurasa wake wa Twitter.
Akizungumzia hatua za kumpandisha cheo kutoka kuwa Luteni Jenerali hadi kuwa Jenerali kamili, Rais Museveni amesema hatua hiyo ilikuja kutokana na yeye kutenda kosa moja tu ukilinganisha na mema mengi aliyoyafanya na atakayoendelea kuyafanya.