
Mkoa wa Arusha unakadiriwa kuwa na watu zaidi ya milioni mbili huku waliopata Chanjo ya UVIKO 19 mpaka sasa ni asilimia sitini na tisa ya wakazi wa mkoa huo sawa na watu laki nane sabini na mbili elfu mia mbili sitini na
Mratibu wa Chanjo mkoa Arusha akiwa katika kikao na na viongozi wa dini na wa Mila anatumia Nafasi hiyo kuiomba jamii kupata chanjo ya UVICO-19 mapema kabla hawaja pata maradhi hayo,kwani chanjo hiyo haitolewi kwa wagonjwa.
Nao viongozi wa dini na viongozi wa mila na viongozi mbalimbali ngazi ya jamii wanaeleza nafasi yao katika kufikisha elimu sahihi kwa umma,na kusaidia kuondoa dhana potofu juu ya madhara yatokanayo na chanjo hiyo.
Chanjo ya uviko 19 katika mkoa wa Arusha ilizindinduliwa na mkuu wa mkoa John Mongella August 3 2021 ambapo ilianza kutolewa Kwa makundi maalumu na mpaka Sasa inaendelea kutolewa.