
Mwenyekiti mtaa wa Ngurumausi Jonas Jackson anabainisha kuwa ajali hiyo imetokea wakati ambapo vijana hao waliofariki walikuwa wanafanya shughuli za upakiaji katika machimbo hayo ya Moramo na kwambwa walikuwa wamejipumzisha ndipo wakafukiwa na kifusi.
Diwani wa Kata ya Mwivaro Philemoni Mollel amewataka wachimbaji wa mgodi huo kutopumzika katika maeneo hayo mara baada ya kazi kwa kuwa sio salama kwa Maisha yao.
Baadhi ya wakazi wa maeneo hayo wameiomba serikali kuweka miundombinu itakayosaidia shughuli za uchimbaji ili kuepusha madhara yanayotokea mara kwa mara.
Miezi Kadhaa nyuma mgodi huu ulifungwa na mkuu wa wilaya ya Arusha Saidi Mtanda mara baada ya watu wengine kufariki kwa kufukiwa na kifusi.