Monday , 10th Oct , 2022

CEO wa lebo ya Kondegang Harmonize amefunguka baada ya taarifa ya kuwatena wasanii wake Killy na Cheed akieleza kwamba anawaamini hawatomuangusha pia wana kila sababu ya kuwa wasanii wakubwa.

Picha ya Harmonize na Cheed na Killy

Akitoa taarifa hiyo kwenye Insta Story yake Harmonize ameandika kwamba "My brother Killy na Cheed, mna kila sababu ya kuwa wasanii wakubwa katika hili Taifa bila shaka nji ni nyeupe nawaaminia sana"

"Nina imani hamtoniangusha, video 2 zilizopo ndani kwa gharama ya Management zilizoongozwa na Travellah zikawe mwanzo wenu mwingine mwema". 

Killy na Cheed wamedumu kwa miaka miwili Kondegang tangu wakitokea lebo ya Kings Music ya Alikiba.