Sunday , 23rd Oct , 2022

Miji iliyoko Pwani ya Pasifiki ya Mexico inajiandaa kwa kimbunga kikali kiitwacho Roslyn chenye nguvu, huku kukiwa na tahadhari kwamba kinaweza kuleta ongezeko hatari la dhoruba na mafuriko. Huduma za dharura za ndani zimekuwa zikifanya maandalizi ya dakika za mwisho.

 Kimbunga Roslyn kinatarajiwa kutua leo katika jimbo la Magharibi la Nayarit, ambalo ni makao ya hoteli maarufu za ufukweni.

Kimbunga hicho kinafungasha upepo hadi 125mph (205km/h), lakini kimeshushwa kutoka Jamii ya 4 hadi Jamii ya 3 na Kituo cha Taifa cha Kimbunga cha Marekani (NHC)..

Mamlaka katika miji ya Nayarit, Jalisco na majimbo mengine kadhaa yamekuwa yakiweka malazi .

Msimu wa kimbunga nchini Mexico kawaida hudumu kuanzia Juni hadi Novemba, na kuathiri pwani zote za Pasifiki na Atlantiki za nchi hiyo.

Mwezi Mei, watu 11 waliuawa baada ya kimbunga Agatha kushambulia kusini magharibi mwa jimbo la Oaxaca.