
Katika hotuba yake ya kwanza kama waziri mkuu Sunak anasema daima atamshukuru Boris Johnson kwa mafanikio makubwa katika utawala wake huku akisisitiza kuwa serikali yake itakuwa na uadilifu, weledi na uwajibikaji
Sunak ameeleza kuwa katika utawala wake anakwenda kuliunganisha taifa hilo na sio kwa maneno tu lakini kwa vitendo huku akieleza kuwa anakwenda kufanya maamuzi magumu kwa faida ya taifa hilo
"Nitajaribu kurekebisha makosa yaliyofanywa na mtangulizi wangu, kurejesha imani katika siasa lakini na kutakuwa na maamuzi magumu mbeleni" amesema Sunak