
Jeshi la wananchi wa Tanzania JWTZ - Kamandi ya Anga
Akizungumza katika hafla ya kufunga zoezi hilo mgeni rasmi Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Innocent Bashungwa amelipongeza Jeshi la Anga kwa ukakamavu na hari thabiti katika zoezi hilo.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya hiyo Shaibu Ndemanga ameiomba serikali kurudisha kambi kubwa ya Jeshi kwa dhumuni la kuimarisha ulinzi kwani mkoa huo unataraji kupokea miradi mingi mikubwa kama mradi wa kuchakata gesi asilia LNG, mradi utakaowekeza Zaidi ya Shilingi Trilioni 70.
Ndemanga amezungumza hayo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, pia amesema endapo Jeshi litarudisha kambi wilayani hapo, wote watakaolenga kuhujumu mradi kiusalama watashindwa kwa kuwa anaamini hali hiyo itadhibitiwa haraka.
Naye Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la Anga nchini Meja Jenerali Shabani Baraghashi Mani akieleza dhumuni kuu la kufanya Mazoezi hayo.