
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Suzan Kaganda
IGP Wambura ametoa maagizo hayo leo Oktoba 28 2022, wakati akimuapisha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Suzan Kaganda kuwa Kamishna wa Polisi na Kamishna wa Kamisheni ya Utawala na Menejimenti ya Rasilimali watu baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Samia Suluhu Hassan kumpandisha cheo na kumteua kwenye nafasi hiyo 24 Oktoba 24, 2022.
Aidha Kaganda ameagizwa kusimamia weledi kwa kuhakikisha kuwa maafisa., wakaguzi, askari na watumishi raia wa Jeshi Ia Polisi wanapata mafunzo ya kujiendeleza mara kwa mara ili kufanya kazi kwa ufanisi sambamba na kuhakikisha anapanga majukumu kulingana na ujuzi, uwezo na elimu na sio kwa upendeleo.
Pia IGP Wambura ametaka kuboreshwa na kuimarishwa kwa uhusiano baina ya Jeshi Ia Polisi na taasisi zingine, pamoja na kuboresha muundo wa mifumo ya kazi za kiutawala kutoka analojia kwenda dijitali.
Kamishna Kaganda anakuwa Kamishna wapili mwanamke kushika nafasi ya ukamishna kwa Jeshi la Polisi tangu Tanganyika ipate Uhuru akitanguliwa na Kamishna Elice Mapunda, aliyekuwa Kamishna wa Kamisheni ya uchunguzi wa Kisayansi Mwaka 2015 hadi mwaka 2017.