
Kamanda wa TAKUKURU mkoa Tanga Zainabu Bakari
Awali akitoa taarifa kwa waandishi wa habari ofisini kwake, Kamanda wa TAKUKURU mkoa Tanga Zainabu Bakari, amesema walibaini udanganyifu huo baada ya uchunguzi na kugundua watoa huduma za afya wilayani Muheza wanahusika na kusajili majina hewa ya wagonjwa wa Virusi vya Ukimwi ili kuzidisha takwimu za ugonjwa huo kwa maslahi yao binafsi.
Alisema wahudumu wa afya wanaohusika na zoezi la kusajili na kuwafuatilia watu wanaoishi na VVU wilayani humo, wamekuwa wakilipwa posho ya gharama ya usafiri na mawasiliano kiasi cha sh. 20,000 kwa siku kila wanapowatembelea wagonjwa hao.
Aidha amesema idadi hiyo ya wagonjwa iliondolewa kwenye mifumo na wahusika waliohusika na usajili wa wagonjwa hewa walipewa barua na kujieleza kwa kitendo cha kusajili wagonjwa hewa ambapo Wizara ya Afya imetoa maelekezo ya kufanya uhakiki kwa wateja wanaotumia dawa ambao sio halisi.