Monday , 14th Nov , 2022

Wazee na Mashirika ya kuhudumia Wazee mkoa wa Kigoma, wamesisitiza Serikali kukamilisha mchakato wa sheria inayosimamia haki za wazee na kuhakikisha wazee wanapata huduma kwa ukamilifu kulingana na mahitaji yao ikiwemo pesheni kwa wazee

Hayo yamejili katika kikao cha baraza a wazee ngazi ya mkoa kilichofanyika mjini kasulu kwa lengo la kujadili maswala ya wazee na kufuatilia shughuli na huduma zilizofanyika katika kipindi cha july na september mwaka huu.

Kwa upande wake afisa miradi shirika la endeleza wazee mkoa Kigoma EWAKI Ruvako Victor amesema uwepo wa sheria ya wazee itapunguza vitendo vya ukatili kwa wazee huku afisa ustawi wa jamii mkoa wa Kigoma Petro Mbwanji akibainisha kuwa uwepo wa sheria hiyo ni hatua ya kuwafanya wazee kupata huduma muhimu kwa ukamilifu