Thursday , 17th Nov , 2022

Mama na dada wa mwandishi mashuhuri wa Uingereza na Misri na mwanaharakati wa demokrasia, Alaa Abdel Fattah, wanatarajiwa kumtembelea baadaye hii leo  kwa mara ya kwanza tangu alipoacha kunywa maji mapema mwezi huu.

Siku ya Jumanne, familia ilipokea barua kutoka kwake ikisema kwamba amevunja mgomo wa kula aliouanza mwezi Aprili, na ataelezea kila kitu katika ziara yao ya kila mwezi ijayo.

Bw Abdel Fattah alikataa chakula kwa matumaini kwamba angalau kingemsaidia kupata ziara kutoka kwa wanadiplomasia wa Uingereza  ingawa hii haikuruhusiwa kamwe.

Uingereza, pamoja na mataifa mengine kadhaa, imetoa wito wa kuachiliwa kwake mara moja.