
Zoezi hilo ni kufuatia kauli ya waziri wa nchi ofisi ya makamu wa rais muungano na mazingira Selemani Jafo aliyoitoa hivi karibuni katika hifadhi ya taifa ya Ruaha mara baada ya kujionea mto Ruaha mkuu kukauka takribani miezi mitatu sasa na kupelekea athari kubwa kwa wanyama,na sasa
Utekelezaji wa zoezi hili la kubomoa mifereji isiyo rasmi na kuchepusha maji linafanyika katika bonde la usanga na ihefu wilayani Mbalali ambako kilimo cha umwagiliaji kimeendelea kushamiri na kuathiri mtiririko wa maji katika mto ruaha mkuu ambao ni tegemeo kwa wanyama katika hifadhi ya taifa ya Ruaha