Tuesday , 6th Dec , 2022

Shehena ya kwanza ya nafaka, ikiwa sehemu ya jitihada ya binafsi ya Ukraine kwa kusambaza kwa mataifa yenye uhataji imewasili nchini nchini Djibouti ikiwa tayari kwa ajili ya kwenda katika taifa jirani la Ethiopia ambalo limekumbwa na ukame mkubwa.

Ubalozi wa Ukraine nchini Ethiopia umethitibisha kwamba nafaka kiasi cha tani 25,000 ni tofauti na jitihada za Umoja wa Matiafa na Mpango wa Chakula Duniani, ambazo zimekuwa zikifanikisha ufadhili wa chakula kutoka Ukraine.

Meli ya pili yenye tani 30,000 za ngano itakuwa inaelekea Ethiopia juma lijalo, huku meli ya tatu ikipakiwa kwa sasa tani 25,000 za ngano ili baadae ziende Somalia.

Ikiwa jitihada za kukabiliana na njaa dunia Ukraine imepanga kupeleka zaidi ya meli 60 katika mataifa kama Ethiopia, Sudan, Sudan Kusini, Somalia, Congo, Kenya,Yemen na kwengineko.