Wednesday , 7th Dec , 2022

Serikali kupitia tume ya haki za binadamu na utawala bora imeyataka mashirika yasiyo ya kiserikali yanayojihusisha na utetezi wa haki za binadamu kufuata sheria kanuni na taratibu ambazo nchi imejiwekea ili kulinda utu na utamaduni wa mtanzania.

Onesmo Ole Ngurumwa mratibu wa kitaifa THRDC

Kauli hiyo imetolewa na katibu mtendaji Patience Ntwina ambaye amesema kumekuwepo na mashirika mengi ambayo mengine kwa makusudi kabisa yanavunja na kukiuka sheria za nchi kwa masilahi ya wafadhili wao ivyo kuwataka sasa viongozi katika mashirika kutazama upya mitazamo na mienendo yao hasa katika kipindi hiki.

Kwa upande wake mwenyekiti wa baraza la mashirika yasiyo ya kiserikali la taifa Lilian Badi amezitaka NGOS kushiriki ajenda za kiserikali huku akizitaka kuzingatia usajili wao sio kudandia na kutangatanga na ajenda kila ajenda mitandaoni.

Kuelekea kilele cha kupinga ukatili wa kijisinsi watetezi wa haki za binadamu kutoka mikoa yote ikiratibiwa na mtandao wa kutetea haki za binadamu Tanzania THRDC na wenzao wa Uganda kwa ujumla wamekutana kujadili mazingira ya kiutendaji katika nchi zao na namna wanavyoshiriki kutatua changamoto za utetezi kwenye nchi husika.