Friday , 9th Dec , 2022

Taasisi ya Tulia Trust Mkoani Mbeya kwa kushirikiana  na Taasisi ya Bilal Muslim Mission Tanzania wameanza kutoa matibabu ya macho bure kwa wananchi wote wa Mkoa wa Mbeya ikiwa ni pamoja na oparesheni ndogo ya macho, kutoa miwani bure na uchunguzi wa awali wa mtoto wa hicho

Meneja wa Taasisi ya Tulia Trust, Jackline Boaz amesema wameamua kutoa huduma hiyo bure ili kuwasaidia wananchi wasioweza kumudu gharama za matibabu ya macho

Amesema huduma hiyo matibabu ya macho ni jitihada za Spika wa Bunge na Mbunge wa Jimbo la Mbeya, Dk. Tulia Ackson kuwasaidia wananchi wake

Huduma ya macho inatolewa kwa siku tatu mfululizo kuanzia Decemba 9 mpaka 12 katika Shule ya Msingi Ruanda Nzovwe jijini Mbeya