
Timu za wataalamu na mbwa wa upekuzi zipo eneo la tukio, kufuatia kuanguka huko St Helier Jana asubuhi.
Serikali ya Jersey inasema juhudi za utafutaji bado zinaendelea. Afisa mkuu wa polisi wa kisiwa hicho Robin Smith alielezea eneo la tukio katika barabara ya gati kama ni tukio la kufedhehesha.
Video iliyotumwa na serikali ya kisiwa hicho, inaonyesha rundo la vifusi na gari lililopondwa .
Serikali ya Jersey imesema timu za wataalamu kutoka Uingereza zimewasili kusaidia wafanyakazi wa ndani katika kutafuta manusura.
Timu ya Kukabiliana na Eneo la Hatari Kusini Magharibi imewasili kisiwani humo, pamoja na Timu ya Utafutaji na Uokoaji ya Mjini kutoka Hampshire & Isle of Wight Fire & Rescue Service.