
Kwa sasa timu hiyo ipo chini ya Kaimu Kocha, Kali Ongala ambaye ameweka rekodi ya kuiongoza timu hiyo kwenye mechi 8 mfululizo za ligi kwa kushinda zote na kukomba pointi 24.
Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Ofisa Habari wa Azam FC Hasheem Ibwe, amesema kuwa kwa sasa wataendelea kufanya kazi na Ongala kwa kuwa amekuwa na mwendelezo mzuri.
“Mtendaji Mkuu wa Azam FC, (Abdulkarim Amin) alimaliza kuhusu ujio wa kocha, Ongala amekuwa na mwendo mzuri na hilo tunajivunia hata msaidizi wake Agrey Morriss wamekuwa wakienda sawa na falsafa za wachezaji.
“Ukweli ni kwamba mpaka sasa kuna CV za makocha wenye uwezo zaidi ya sita na kati ya hizo wawili ni wazawa hivyo mambo yakiwa sawa kila kitu kitakuwa wazi,” amesema Ibwe.
Ongala ambaye amebea mikoba ya kuinoa Azamm FC, Desemba 9,2022 alikiongoza kikosi hicho kushinda mabao 9-0 dhidi ya Malimao kwenye mchezo wa raundi ya Pili, Kombe la Shirikisho.