Wednesday , 28th Dec , 2022

Klabu ya Tanzania Prisons SC yawekewa Tsh. Milioni 30 endapo kama wataifunga Simba SC kwenye mchezo wa Ligi kuu NBC,utakaopigwa kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, Desemba 30, 2022 majira ya saa moja usiku.

Bonasi hiyo imetolewa wadhamini wao ambao ni kampuni ya usafirishaji, Silent Ocean na Kilimanjaro Star Cargo endapo wataifunga Simba katika mchezo wa mzunguko wa pili baada ya kupoteza raundi ya kwanza wakiwa Uwanja wa Sokoine, bao la Wanamsimbazi lilifungwa na Jonas Mkude.

Akizungumza na waandishi wa habari Katibu wa timu hiyo, Ajibu Kifukwe amesema wadhamini hao wameweka pesa sehemu sahihi na kwamba wanaongeza chachu ya ushindani Ligi Kuu Bara, akiamini hilo litawafanya wachezaji wajitume kwa bidii kwamba kuna kifuta jasho.

"Tunaiheshimu Simba hilo halijifichi, lakini kama tuweza kupata nao sare Ile ambayo ilikuwa na kina Luis Miqussoine hii tutapambana nayo hadi kieleweke huku wakiahidi kuonesha mchezo mzuri na kupata matokeo''amesema Ajibu Kifukwe.

Nae Nahodha wa Prisons, Benjamin Asukile alisema kwa niaba ya wachezaji wenzake kwamba wapo tayari kwa ajili ya kuipambania timu yao, akikiri morali imeongezeka zaidi baada ya kupewa bonasi nono na wadhamini wao, Silent Ocean.