
Mradi huo ambao unagharimu jumla ya shilingi bilioni 76.9 utakaotekelezwa katika Mikoa 8 hapa Nchini ambapo kati ya fedha hizo shilingi bilioni 11.5 zitatumika kwa jili ya utekelezaji wa mradi huo Mkoani Tanga
Kufuatia mradi huo Wakandarasi wamesisitizwa juu ya umuhimu wa kununua vifaa kutoka kwa kampuni za ndani ya nchi ili kuimarisha uchumi wa Tanzania huku baadhi yao wakitakiwa kuacha tabia ya kununua bidhaa nchi za nje bidhaa ambazo zinapatikana hapa nchini jambo ambalo linasaidia kuimarisha uchumi wa nchi nyingine
Kaimu Mkuu wa Mkoa Tanga Hashim Mgandilwa ameyasema hayo wakati wa makabidhiano ya mkataba wa utekelezaji wa mradi wa usambazaji wa umeme wa Rea katika maeneo ya pembezoni mwa miji kwa mkandarasi kutoka kampuni ya OK ELECTICAL & ELECTRONICS SERVICE.
Mgandilwa amesema kuwa kumekuwa na tabia ya baadhi ya wakandarasi kununua bidhaa nchi za nje bidhaa ambazo zinapatikana hapa nchini jambo ambalo linasaidia kuimarisha uchumi wa nchi nyingine.
Aidha amesisitiza juu ya mkandarasi aliyepewa kazi, kuajiri wafanyakazi kutoka kwenye maeneo ambayo mradi huo unatekelezwa ili kusaidia kuajiri vijana katika kazi ambazo sio za kitaalamu.
"Serikali ya awamu ya sita ya Rais Samia Suluhu Hasan imedhamiria kukuza uchumi wa nchi na mtu mmoja mmoja kwa kuweka miradi mingi ikiwemo huu uwekaji wa miundombinu ya umeme katika jamii yetu hususani maeneo ya pembezoni mwa miji kwa kuzingatia ubora wa nishati, "alisema Mgandilwa.
"Ninaomba kuwataka wakandarasi kama tulivyosikia hapa mradi huu unatekelezwa Tanga tunatamani tuone vibarua wote au ajira izile ambazo haziitaji taaluma tunaomba na tunawataka vibarua hao watoke kwenye maeneo husika ya mradi unapotekelezwa kumekuwa na kasumba baadhi ya wakandarasi wanatembea na watu wanatoka nao huko kwenye maeneo walikotoka na kuacha vijana wengi waliopo kwenye maeneo husika, "alisistiza.