Wednesday , 4th Jan , 2023

Matokeo ya darasa la nne nchini yametangazwa ambapo Jumla ya wanafunzi 1,320,700 kati ya 1, 592, 235 wenye matokeo sawa na asilimia 82.95 wamefaulu mitihani upimaji wa kitaifa wa darasa la nne kwa kupata madaraja A, B, C D.

Kati yao wasichana ni 694, 547 sawa na asilimia 84.76 na wavulana ni 626,153 sawa na asilimia 81.03
Kuhusu wanafuzi waliofanya mitihani ya marudio darasa la saba

Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta), limesema wanafunzi 2,095 kati ya 2,180 waliofanya mtihani wa marudio wa darasa la saba baada ya kufutiwa matokeo ya awali wamefaulu daraja A hadi C sawa na asilimia 96.1

Wanafunzi hao ni kati ya 2,194  waliofutiwa matokeo ya mtihani huo na Necta baada ya kubainika kufanya vitendo vya udanganyifu uliofanyika Oktoba 5, 6 mwaka 2022

Hata hivyo katika matokeo hayo somo la Kiingereza asilimia 79.89 ya watahiniwa wote wamepata daraja D na E huku asilimia 82.09 ya watahiniwa wote wakipata daraja D na E katika somo la hisabati

Ufaulu wa jumla umeshuka kutoka asilimia 86.30 mwaka 2021 hadi kufikia asilimia 82.95 mwaka 2022

Kwa upande wa kidato cha pili jumla ya Wanafunzi 539,645 kati ya 633,537 wenye matokeo ambao ni sawa na 85.18% wamefaulu ambapo wamepata Madaraja ya 1, Ill na IV.

Kati yao Wasichana ni 283,541 sawa na 83.05% na Wavulana ni 256,104 sawa na 87.67%, 
Mwaka 2021 Wanafunzi waliofaulu walikuwa 555,857 sawa na 92.32%

KUTAZAMA MATOKEO KIDATO CHA PILI>  BONYEZA HAPA 

MATOKEO DARASA LA NNE> BONYEZA HAPA 

MATOKEO DARASA LA SABA (MARUDIO)> BONYEZA HAPA