Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Walioiba mafuta ya SGR wahukumiwa

Thursday , 26th Jan , 2023

Mahakama ya wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza imewahukumu kwenda jela miaka miwili au kulipa faini washtakiwa watatu kati ya sita waliohusika na wizi wa mafuta ya petroli yaliyokuwa yanatumika katika ujenzi wa reli ya kisasa SGR 

Akisoma hukumu hiyo hakimu mkazi mwandamizi wa mahakama hiyo John Jagadi amesema washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka matatu yakiwemo ya kupatikana na mali ya wizi, kufanya biashara ya mafuta bila kuwa na leseni pamoja na kufanya biashara ya mafuta ya petroli katika mazingira hatarishi ambapo washtakiwa hao walikiri makosa mawili 

Katika kesi namba 15 inayomkabili Levy Daniel na Fredy Magay ambao walikamatwa mnamo tarehe 23 na mafuta ya petroli lita nne na wakakiri kosa moja kufanya biashara ya mafuta bila kuwa na leseni

Katika shtaka la kufanya biashara bila kuwa na leseni hakimu Jagadi amesema kwa mujibu wa kifungu namba 132 kifungu kidogo cha kwanza na cha nne cha sheria ya udhibiti wa nishati washtakiwa hao watatakiwa kutumikia kifungo gerezani cha miaka miwili au kulipa faini ya shilingi laki moja kila mtu

Aidha katika kesi nyingine namba 9 ya mwaka huu inayomkabili Dotto Ihanu ambae amekiri kufanya biashara ya mafuta bila kuwa na leseni pamoja na kuuza mafuta ya petroli katika mazingira hatarishi ambapo mnamo tarehe 23 ya mwaka huu wilayani Kwimba alikamatwa na lita 21 za mafuta ya petrol

Katika shtaka la kufanya biashara bila kuwa na leseni mahakama hiyo imemhukumu kifungo cha miaka miwili gerezani au kulipa faini ya shilingi laki moja na elfu hamsini huku katika shtaka lingine la kufanya biashara ya mafuta katika mazingira hatarishi akihukumiwa kwenda gerezani miezi sita au kulipa faini ya shilingi laki moja

Mahakama imesema washtakiwa wote watatu kama wakifanikwa kulipa faini shtaka moja la kupatikana na mali ya wizi lina dhamana na wakikidhi masharti ya dhamana watakuwa huru huku kesi hiyo ikipangwa tena hadi tarehe 9 ya mwezi wa pili mwaka huu.
 

HABARI ZAIDI

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko,

Wadau wa afya simamieni ukusanyaji mapato

Picha za Kuonesha Muelekeo wa Kimbunga IALY

Kimbunga IALY charipotiwa bahari ya Hindi

Mabaki ya Nyumba yenye vyumba 12 iliyoteketea na Moto

Moto wateketeza nyumba yenye vyumba 12

Baadhi ya Majirani wa Kijana Amani Abed ambaye Amejinyonga baada ya kutoka Hospitali.

Kijana ajinyonga baada ya kutoka hospitali

Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani

Marekani yatangaza kulifadhili jeshi la Ukraine

Kaimu Mkurugenzi wa ufuatiliaji na uzingatiaji sheria NEMC,

Wamiliki wa Hospitali nchini wapewa siku 90

Baadhi ya Wakazi wa Kata ya Madanga Mkoani Tanga

Wagoma kubeba mimba kwa kukosa huduma za afya