Thursday , 9th Feb , 2023

Muswada wa Bima ya Afya kwa Wote (UHC), ambao ulikuwa uwasilishwe leo Bungeni Jijini Dodoma umesitishwa tena kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Bungeni na Spika wa Bunge la Tanzania Dk.Tulia Akson

Awali ratiba ya Bunge iliyotolewa Januari 30, 2023 ilionyesha kuwa Muswada huo ulikuwa uwasilishwe Bungeni siku ya leo tarehe 9.02.2023 kwa kufuata hatua zake zote za mchakato wa utungwaji wa Sheria.

Baada ya kipindi cha maswali na majibu kumalizika leo Bungeni Jijini Dodoma Spika wa Bunge Dkt.Tulia Ackson, alisema muswada huo bado unafanyiwa marekebisho na Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.

Katika kipindi cha maswali na majibu ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu leo Bungeni, badhi ya wabunge walitaka kujua hatua ambazo Serikali inazichukua katika kukabiliana na ubadhilifu wa miradi ya Maendeleo ambapo Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa aliliambia Bunge kuwa serikali imeanzisha kitengo cha ufwatiliaji na tathmini kwenye sekta za Serikali ambazo zitabaini mapungufu kabla ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikaali CAG hajafika.

Kuhusu misamaha ya kodi kwa zile bidhaa zinazosamehewa kodi Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amewaonya wafanyabiashara wanaoingiza bidhaa hizo nakuziuza kwa bei ya juu kwani inawanyima haki watu wanaokusudiwa kununua bidhaa hizo kwa gharama ndogo.

Wizara zilizopata nafasi yakujibu maswali na miungozo iliyoombwa na baadhi ya wabunge ni Wizara ya Kilimo kuhusu mgawanyo wa chakula,Wizara ya  Nchi ,Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira kuhusu katazo la usafirishaji wa ndizi kutoka Tanzania Bara kwende Visiwani Zanzibar na Wizara ya Elimu ,Sayansi na Teknolojia kuhusu vyeo wanavyotunukiwa viongozi kutoka kwa baadhi ya bila kuingia darasani kusomea na wizara hiyo inawasaidiaje wahitimu wanaofutiwa mitihani ile hali wanaovujisha ni wafanyakazi wa baraza la mitihani.

Kabla ya shughuli za  Bunge kuisha hii leo  Dk.Tulia Akson alitoa taarifa ya mvutano ulioibuka baina ya baadhi ya wabunge na Waziri wa Fedha na Mipango kuhusu kauli ya Uganga wa kienyeji nakuagiza kauli hiyo iondolewe kwenye kumbukumbu za Bunge hukua akiagiza majibu ya staha ndio yatumiwe.