Mwanafunzi huyo anaefahamika kwa jina la Raulence Nicholous (16 ) alituhumiwa kuiba maandazi matano katika duka la shule.
Mapema february 12,2023 watumishi hao wawili wa shule hiyo walipobaini maandazi hayo matano yenye thamani ya sh 1500 yamepotea,ndipo walipotoa adhabu hiyo kali kwa mtoto huyo.
Waliohusika na tukio hilo baada ya kuona hali ya mwanafunzi huyo waliemcharaza fimbo si shwari walimkimbiza hospital ya Ifisi kwa ajili ya matibabu.
Pia kamanda wa polisi amebainisha sababu ya mtoto huyo kuiba maandazi hayo kuwa ni njaa huku akilaani vikali adhabu iliyotolewa ,na upelelezi wa shauri hili ukikamilika watuhumiwa watafikishwa mahakamani.
Baadhi ya wananchi Mkoa wa Mbeya wamelaani vikali kitendo cha walimu kuwapa adhabu nzito na za kupindukia wanafunzi mpaka kuwajeruhi.



