Saturday , 18th Feb , 2023

Zaidi ya  wanafunzi 1000 wa Shule ya Msingi Kerege iliyopo Bagamoyo mkoani Pwani wamefanyiwa vipimo vya magonjwa mbalimbali ikiwamo Malaria, Macho  na Meno sambamba na kupatiwa  matibabu bure yaliyoandaliwa na Rotary Club of Dar es salaam-Oysterbay kwa kushirikiana na madaktari.

Aidha wanafunzi hao wamepatiwa elimu ya Afya huku Rais wa Club hiyo Krutin Shah akisema kuwa utoaji wa elimu na matibabu bure ni moja ya mikakati yao ya kukabiliana na magonjwa tangu walipoanzisha kambi za matibabu mwaka 2012.

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kerege, Esther  Awino amewaomba wazazi kushirikiana na walimu katika kutatua changamoto za kiafya zinazowakumba wanafunzi ili waweze kusoma katika misingi bora.

Nao baadhi ya wazazi wamesema kuwa matibabu hayo yamewasaidia kwa kiasi kikubwa kwani wameweza kujua afya za watoto wao na kuwataka wazazi wengine kuhakikisha wanawapeleka watoto kujua afya zao.