Wizara ya ulinzi ilithibitisha kuwa kombora hilo limezinduliwa leo Jumamosi,na liliruka kwa dakika 66 na kutua katika Bahari ya Japani. Hii ni baada ya Pyongyang kuonyesha uwezo wake mkubwa wa kijeshi katika gwaride lililojumuisha zaidi ya dazeni za silaha za ICBM.
Siku ya Ijumaa, Korea Kaskazini juu ya mazoezi yaliyokua ya kijeshi kati ya Korea Kusini na Marekani.
Mazoezi ya kila mwaka ya ambayo yanatarajiwa kuanza mwezi ujao, yanalenga kusaidia kuondoa ongezeko la vitisho vya nyuklia vya Korea Kaskazini.
Lakini Pyongyang kwa muda mrefu imekuwa ikisisitiza kuwa mazoezi hayo yako katika maandalizi ya kuivamia Korea Kaskazini.
Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida amesema Kombora la Jumamosi, ambalo ni la kwanza kurushwa tangu siku ya mwaka mpya, lilianguka magharibi mwa Hokkaido, katika eneo la kipekee la kiuchumi la Japani (EEZ) .
EEZ ni eneo la bahari ambalo nchi ina mamlaka juu yake. Japani ni eneo la maili 200 kutoka pwani yake.



