Mkuu wa wilaya ya Geita akiwa na Jeshi la Polisi pamoja na wanafamilia
Baadhi ya ndugu na shuhuda wa tukio hilo wanaelezea jinsi Watoto hao walivyoingia kwenye nyumba na kuanza kumpiga sehemu mbalimbali na kumkata kichwa mama huyo aliekuwa mjamzito.
Mwenyekiti wa kitongoji cha Kilimahewa anasema waliotekeleza mauaji hayo ni Watoto wa baba mwenye mji kwa mama mwingine ambao pia walimjeruhi baba yao kwa kumchoma na visu ambae kwa sasa yupo hospital anapatiwa matibabu.
Mkuu wa wilaya ya Geita Cornel Magembe amefika katika tukio hilo na kuzungumza na wafiwa pamoja na waombolezaji huku akikemea mauaji ya kinyama na kuliagiza Jeshi la Polisi kudhibiti matukio ya mauaji na ujambazi.
Tazama video ya tukio hapo chini



