Kimbunga hicho chenye nguvu kilitua katika nchi jirani ya Madagascar siku ya Jumanne, ambako kilisababisha vifo vya watu watano, na kinatarajiwa kuongezeka kabla ya kupiga kusini mwa Msumbiji siku ya Ijumaa.
Majimbo ya mikoa ya Sofala, Inhambane, Manica na Gaza ndiyo yaliyo hatarini zaidi, kwa mujibu wa maafisa.Tahadhari imetolewa na shirika la kitaifa la usimamizi wa hatari ambalo linaruhusu shughuli za kukabiliana na majanga kuharakishwa.
Mvua kubwa tayari imesababisha mafuriko katika baadhi ya maeneo ya nchi na mamlaka inasema mvua ya ziada kutokana na kimbunga hicho inaweza kuathiri hadi watu milioni 1.75
Nchini Zimbabwe, maafisa wamesema watafunga shule siku ya Ijumaa katika maeneo ambayo huenda yakaathirika. Watu pia wameonywa dhidi ya kuvuka mito iliyojaa wachimbaji kuonywa dhidi ya kwenda chini ya ardhi.
Kimbunga hicho kinatarajiwa kuleta upepo mkali na mvua kubwa mashariki mwa Zimbabwe.





