Baba huyo ametengana na mama yao mzazi miaka saba iliyopita kutokana na kumfanyia vitendo vya ukatili vikiwemo vipigo.
Akisimulia alivyopata taarifa ya tukio hilo mama mzazi wa watoto hao ambao wanasoma shule ya msingi Mapinduzi, amesema alipata mshituko baada ya kuona askari na viongozi wa Mtaa nyumbani kwake anapoishi kwa sasa baada ya kuachana na mzazi mwenzie miaka saba iliyopita na kuelezwa juu ya tukio la watoto kudaiwa kulawitiwa na baba yao mzazi kitendo ambacho kimemuumiza na kuiomba serikali kuchukuwa hatua kali ili liwe fundisho kwa wenye tabia kama hiyo.
"Nimeumia sana nahisi maumivu makali ambayo siwezi hata kusimulia,naiomba serikali ichukuwe hatua kali kwa mwanaume huyo,watoto wangu walikuwa wakija kunitembelea nawauliza kama kuna shida hawasemi lakini yule mkubwa alikuwa anajinyea nikampigia simu baba yao akasema anaumwa na dawa ya kumtibu ni ya kienyeji kumbe alikuwa ananidanganya anawachezea watoto wangu anawalawiti"anasema mama huyo(jina limehifadhiwa).
Kwa upande wake Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga Janeth Magomi amethibitisha kutokea tukio hilo na tayari wanamshikilia mtuhumiwa kwa hatua zaidi za kisheria huku akiiomba jamii kuendele kuwafichuwa watu wanaofanya vitendo vya ukatili wa kijinsia huku akilaani vikali kitendo walichofanyiwa watoto hao na baba yao mzazi .




