Thursday , 9th Mar , 2023

Jeshi la Kujenga Taifa JKT limewataka vijana wanaohitimu mafunzo ya kijeshi, kuacha tabia ya kuilalamikia aerikali kwa kuacha kutoa ajira, badala yake Watumie stadi za maisha ujuzi waliopatiwa vikosini, kuibua fursa za ajira binafsi ambazo zinawasaidia kukuza uchumi wao na Taifa

Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Mafunzo na Oparesheni Jeshi la Wananchi, Brigedia Jenerali Charles Ndiege kwa Vijana wanaohitimu mafunzo ya Kijeshi katika kambi ya 821 KJ Bulombora iliyopo Wilaya ya Kigoma Mkoani Kigoma
Brigedia Jenerali Charles Ndiege amewataka vijana kuibua ajira binafsi na kuacha kutoa malalamiko kwa Serikali kuwa haitoi ajira


Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Salum Kalli amewataka Vijana waliohitimu Mafunzo, kuwa wazalendo kwa Taifa na kutowadhuru Raia wengine, Wakati Kamanda Kikosi Luteni Kanali Juma Hongo akibainisha vijana hao kupata ujuzi wa stadi za maisha na kijeshi kwa ukamilifu. 

Aidha Vijana waliohitimu Mafunzo ya Kijeshi katika kambi ya 821 KJ Bulombora, wameeleza kufanikiwa kukomaa katika masomo ya stadi za maisha na kwamba yatakuwa chachu kuweza kuanzisha shughuli za kujiajiri mara baada ya kuhitimu mafunzo ya Kijeshi