
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara, RPC George Katabazi amethibitisha tukio hilo akidai Machi 23.2023, huko katika Kitongoji cha Njutaa Kijiji cha Kinana, askari Polisi wakiwa Doria walimkamata maneno Yeremia Matantamala (43) akiwa na silaha amebeba akielekea kwenye makazi ya watu
RPC Katabazi amesema Kiini cha kukutwa na silaha hiyo amedaiwa kuitumia kujipatia kipato haramu kwa kuwindia wanyama pori.
RPC Katabazi amesema Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na mara utakapokamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazo mkabili na kutoa wito kwa jamii kuendelea kushirikiana na Polisi katika kukomesha vitendo vya kihalifu.