Thursday , 30th Mar , 2023

Kampuni ya Coca cola Kwanza imenunua na kuzindua gari aina ya Scania yenye mfumo unaotumia gesi asilia ukiwa ni mkakati wa kulinda mazingira kufuatia mabadiliko ya tabia nchi yanayoendelea kuathiri nchi na dunia kwa ujumla.

Gari aina ya scania inayotumia mfumo wa gesi kwa ajiri ya kusafirisha vinywaji

Akizindua gari hiyo ambayo ni kwa ajiri ya kubeba vinywaji kwa masafa marefu Mkurugenzi wa mipango kutoka kampuni ya Cocacola kwanza Hasi Mzee Ally sambamba na meneja maendeleo biashara kutoka Scania Eliavera Timoth wamesema walikuwa katika matumizi ya awali ya gari hilo tangu mwaka 2021 na sasa kama kampuni wamejiridhisha na kuamua kulinunua gari hilo kutoka Scania.

Wadau hao wameiomba sasa serikali kuangalia namna ya kuongeza vituo vya kujazia gesi ilikuondoa misonganoa ambayo inakuwepo wakifurahishwa na mikakatia ya serikali kutoa leseni kwa watu wenye vuo vya mafuta watakaoweza kuweka mifumo ya kujazia gesi asilima kwenye magari.

Amesema utafiti walioufanya matumizi ya gari hilo linaokoa asilimia 27 ya kila safari linalofanya kutoka wakitoa nafasi kwa makampuni ya ndani yenye uwezo wa kutengeneza matanki makubwa ya kuhifadhia gesi ambayo inaweza kwenda na kurudi umbali ambao hakuna vituo vya kujazia gesi