Thursday , 30th Mar , 2023

Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameishukuru serikali ya Marekani kwa msaada wake nchini hasa katika sekta ya afya ambao umesaidia kupunguza maambukizi ya Malaria, UKIMWI na Kifua kikuu

Rais Samia ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wanahabari baada ya kumpokea Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris Ikulu Jijini Dar es salaam

"Kupitia msaada wenu vifo vya malaria vimepungua vimepungua sana kutoka kutoka milioni 7.7 mwaka 2025 hadi milioni 3.5, kwa hiyo tumepunguza zaidi ya nusu na nadhani kwa jitihada zaidi tutapunguza zaidi"

"Katika sekta ya afya UKIMWI na kifua kikuu havitishii tena maisha ya watu wetu, maambukizi ya UKIMWI yameshuka kutoka asilimia 7.2 mwaka 2912 hadi asilimia 4.7 mwaka 2016/17 na imepungua zaidi mwaka 2021" amesema Rais Samia

Aidha Rais Samia amefungua milango ya kujadili mikataba ya visa ili kuweka urahisi wa wananchi wa Marekani na Tanzania kusafiri wao na mizigo yao katika nchi hizo

"Kuna suala la Visa kwa ajili ya kurahisisha usafiri wa watu na mizigo kati ya nchi zetu mbili, na katika hilo Tanzania inakaribisha utayari wa Marekani kufanya mapitio ya mkataba wa sasa wa visa"  

Akizungumza baada ya kupokelewa Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris amesema mabadiliko ya kimaendeleo yanayoendelea Afrika yatainufaisha dunia kwa ujumla huku akisisitiza kuwainua wanawake kiuchumi

"Naamini kwamba kwa mabadiliko na maendeleo  yanayoendelea barani Afrika na Tanzania yatatengeneza kesho nzuri ya dunia na yatanufaisha dunia nzima"

"Wanawake duniani lazima washiriki katika kukuza uchumi, na washiriki kwa usawa hususani kwenye uongozi, ukiinua uchumi wa mwanamke umeinua uchumi wa familia na jamii kwa ujumla" amesema Kamala Harris