Liberation imesema mwandishi wake Agnès Faivre na Sophie Douce wa Le Monde waliwasili Paris mapema Jumapili baada ya kuitwa tofauti kwa mahojiano na mamlaka ya kijeshi siku ya Ijumaa na baadaye kuarifiwa juu ya kufukuzwa kwao.
Kupitia tovuti yake, Liberation imesema kuwa wanabahari wao wwili ni wenye maadili kamili, ambao walifanya kazi nchini Burkina Faso kisheria, na visa halali na vibali na kwamba wanapinga vikali kufukuzwa huku bila haki kabisa.
Hakukuwa na taarifa yoyote kutoka kwa mamlaka nchini Burkina Faso. Wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa haikujibu mara moja ombi la kutoa tamko kutoka kwa shirika la habari la Reuters.
Uhusiano kati ya Paris na Ouagadougou umezorota sana tangu jeshi la Burkina Faso lilipochukua madaraka kwa mapinduzi mwezi Oktoba mwaka jana.




