Tuesday , 16th May , 2023

Baraza la michezo la Taifa BMT Limewatangazia wanachama na wadau wa mchezo wa mpira wa miguu kwa watu wenyewe ulemavu kuwa wapo kwenye maandalizi ya uchaguzi mkuu wa viongozi wa TAFF utaotangazwa hivi karibuni.

Hayo yameeleezwa na Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano BMT  Frank Mgunga amesema kuwa mchakato ambao watauweka katika uchgauzi huo utakuwa umezingatia misingi ya utawala bora katika Michezo.

'' Wadau wowote wenyewe sifa wajitokeze kuchukua fomu pindi tarehe ya uchaguzi itakapotangazwa '' Frank Mgunga

Aidha Mgunga ametoa wito kwa Vyama na Mashirikisho ya michezo nchin kujisajili ili waweze kuwaingiza katika mfumo wa Michezo.