Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Wabunge waipongeza Wizara ya Maliasili

Monday , 29th May , 2023

Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Tanzania wameipongeza Wizara ya Maliasili na Utalii Kwa Kazi nzuri inayoifanya ya kuhifadhi raslimali kwa faida ya vizazi vya sasa na baadaye huku wakisisitiza ushirikishwaji wa jamii zinazozunguka maeneo ya hifadhi.

Waziri wa Maliasili na Utalii Mohamed Mchengerwa, akiwa na Naibu waziri Mary masanja na Katibu Mkuu wake Dkt. Hassan Abbas

Wakichangia hoja zao kwenye semina maalum ya uhifadhi iliyoratibiwa na Wizara ya Maliasili na Utalii leo Mei 29,2023 wabunge hao wamefafanua kuwa katika kipindi  kifupi  kumekuwa  na maboresho makubwa katika uhifadhi wa raslimali ambapo wameomba juhudi zaidi zifanywe ili sekta hizo ziweze kutoa mchango zaidi katika  uchumi wa taifa.

Akizungumza Mbunge Esther Matiko amempongeza Waziri wa Maliasili na Utalii, Mohamed Mchengerwa  kwa kuweza kushughulikia mgogoro wa mipaka  baina ya  hifadhi ya Serengeti na  vijiji vinavyoizunguka hifadhi hiyo kwenye wilaya ya Tarime ambapo amesema njia aliyoitumia ya ushirikishwaji ndiyo njia pekee inayoleta matokea chanya.

Akichangia katika semina hiyo, Mbunge Charles Mwijage ameiomba Wizara kuzingatia sheria na kuondoa mifugo yote ambayo imevamia maeneo mbalimbali ya hifadhi ambapo Mhe. Mchengerwa ametoa siku 14 kuondoa mifugo yote.

Mbunge wa Manyoni Mashariki,  Mhe. Pius Chanya ameishauri serikali kuweka mikakati  kabambe ya kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii ikiwa ni pamoja na kufanya marekebisho makubwa katika mfumo wa taasisi zinazoshughulikia sekta ya utalii kwa  kubadili Bodi ya Utalii kuwa Mamlaka.

Awali akizungumza katika semina hiyo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Mohamed Mchengerwa amesema migogoro mingi inayojitokeza sasa kwenye maeneo ya hifadhi  ni  siyo ya maliasili na utalii bali imezalishwa  na migongano ya sheria ambapo ammewasihi wabunge kuangalia namna bora  ya kutunga sheria zinazokinzana.

Aidha, amesema rasilimali za misitu na nyuki huchangia asilimia 3.3 ya pato la Taifa, asilimia 5.9 ya mapato yatokanayo na biashara ya nje, na ajira takribani milioni 3 za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja. 

Pamoja na faida hizo, hifadhi za wanyamapori na misitu ni muhimu kwa mifumo ikolojia ikiwa ni pamoja na uhifadhi wa bioanuai, kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, hewa safi na kuhifadhi vyanzo vya maji.

Ameongeza kuwa Sekta hizi zinakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo, ujangili, uvunaji haramu wa mazao ya misitu, uchimbaji haramu wa madini, uvamizi wa maeneo ya hifadhi kwa ajili ya shughuli za kulisha mifugo, kilimo na makazi na mioto haramu. 

HABARI ZAIDI

Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa

Maandamano yetu sio kelele za wahuni - Golugwa

Nyumba ambayo mwili wa mwanaume ulikaa hadi kuharibika

Mke aishi na maiti ya mumewe akiamini atafufuka

Ofisa wa idara ya manunuzi na mikataba akimpatia maelezo mmoja wa wananchi wawaliojitokeza kutembelea banda la GGML katika maonesho ya OSHA na kujifunza namna kuzingatia usalama katika shughuli zao za kila siku.

GGML yaja na teknolojia za kisasa za uokoaji

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Rais Samia asema CDF mwanamke atapatikana 2030

Mratibu wa idara ya dharura (ERT) kutoka GGML, Mohamed Mwaimu akimuonesha mama lishe namna ya kuzima moto wakati inatopokea mtungi wa gesi unapopata hitilafu na kulipuka. Mafunzo hayo yametolewana GGML kwa kushirikiana na OSHA kwa akina mama lishe 50 wa mkoani Arusha.

Mama lishe wafundishwa kulikabili janga la moto

Picha ya AY kulia na Mr II Sugu kushoto

AY Starring wa muziki wa BongoFlava