
Rais Dk Samia ameyasema hayo jijini Dar es salaam wakati wa hafla ya kupokea ndege ya mizigo ya Air Tanzania aina ya Boeing 767-300F ambapo amewataka watanzania kuendelea kuwaombea viongozi wa serikali ili waendelea kufanya kazi na kutatua kero za wananchi.
Kwa upande wake waziri wa ujenzi na uchukuzi Profesa Makame Mbarawa amesema serikali kupitia wizara ya ujenzi itaendelea kuboresha sera, sheria pamoja na masuala mengine ili kuweka mazingira bora ya usafiri hasa sekta ya anga
Naye mkurugenzi wa shirika la ndege la Tanzania mhandisi Ladslaus Matindi amesema ATCL imepiga hatua baada ya mageuzi yaliofanywa na serikali ambapo mpaka sasa imeweza kuleta ndege 13 kati ya 20 zinazo hitajika huku wakiomba serikali kuongeza ndege ya mizigo kutokana na kampuni hiyo kusaini mikataba na mashirika makubwa ili kufanya usafirishaji wa mizigo.
Ndege ya boeng 767 _ 300 F inauwezo wa kubeba tani 54 za mizigo na hivyo kuja kutatua changamoto ya uhaba wa ndege ya mizigo kutokana na Tanzania kuzalisha zaidi ya tani 24 za mizigo inayo paswa kwenda nje