Sunday , 2nd Jul , 2023

Mkuu wa Mkoa wa Dsm Albert Chalamila amewataka wananchi wa Mtaa wa Mbopo kata ya Mabwepande dsm ambao walivamia na kujenga Makazi yao katika Ardhi inayomilikiwa Kihalali na Shirika la Maendeleo la Mkoa wa Dsm DDC kutokubali kudanganywa na baadhi ya wanasiasa au Wanasheria wababaishaji

Mkuu wa Mkoa wa Dsm Albert Chalamila akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Mbopo kata ya Mabwepande.

Chalamilka ametoa kauli hiyo katika Mkutano uliofanyika katika Mtaa wa Mbopo ambapo amesema baadhi ya watumishi wa Umma hasa katika kitengo cha ardhi katika manispaa ya Kinondoni kwa kushirikiana na baadhi ya wevyeviti wa Serikali za Mitaa hawakuwa waadilifu kwa kuuza na kutoa hati juu ya Ardhi yenye hati.

Katika Mkutano huo baadhi ya wananchi wamesema katika Kipindi kirefu walikuwa wakiishi kwa Mashaka kutokana na tishio la kubomolewa nyumba zao kutokana na kesi zote walizofungua mahakamani kushindwa lakini wakafarijika baada ya DDC kukaa nao na kuweka Mpango wa maridhiano na Kupimiwa ili kila Mwananchi alipe kigogo kidogo katika eneo analolimiliki.

Hata hivyo Chalamila alihitimisha Mkutano huo kwa kuwataka wananchi hao kuwa wakweli na kujiepusha na Makundi yanayowapotosha na kujipatia fedha na kuweka rehani Maisha yao badala yake wakubaliane na Mpango wa maridhiano na Shirika hilo kwa kupimiwa na kulipia ardhi kwa gharama kidogo ili Waendelee kuishi katika makazi yao.