Thursday , 12th Oct , 2023

Benki ya DTB Tanzania katika kuadhimisha siku ya mtoto wa kike duniani wamechangia kampeni ya Namthamini taulo za kike zenye thamani ya Tsh milioni 10.

BW. Ravnet Chowdhury akikabidhi taulo za kike kwa wanafunzi wa shule ya msingi Mashujaa.

Kampeni ya Namthamini ya East Africa TV na East Africa Radio kila mwaka hukusanya taulo za kike kutoka kwa wananchi na wadau mbalimbali na kuzifikisha kwa wanafunzi wa kike wanaotoka kwenye mazingira magumu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DTB Tanzania, BW. Ravnet Chowdhury alisema ''wasichana wa shule watakaonufaika na mchango huu sio tu kwamba wataweza kuhudhuria masomo bila kusimama kipindi cha hedhi, pia utaboresha viwango vyao usafi kwa kiasi kikubwa''.