Sunday , 15th Oct , 2023

Mkuu wa wilaya ya Mufindi mkoani Iringa Dkt. Linda Salekwa amewataka wananchi wa wilaya hiyo kuchangamkia fursa ya biashara ya kuvuna utomvu wa miti ya mbao laini (pine) ili kukuza kipato chao

Dkt. Seleka ameyasema hayo Mwishoni mwa juma alipokuwa katika kiwanda cha Mastan Solution Company Limited kinachojihusisha na uvunaji wa utomvu huo na kusafirisha nje ya nchi kama malighafi za viwandani 

Dkt. Salekwa amesema licha ya Kiwanda hicho kufanya kazi nzuri ipo haja ya kuanzishwa kiwanda kingine ambacho kitafanya uzalishaji wa awali tofauti na ilivyo sasa ambapo malighafi inasafirishwa kwenda nje ya nchi.

"Natamani tufike mbali si kuuvuna utomvu tu na kuusafirisha kama malighafi ,ningependa itafutwe namna ama Teknolojia itakayokuwa na uwezo wa kutengfeneza vitu mbalimbali ambavyo vinatokana na utomvu huu'' Alisema Dkt. Salekwa

Dkt Saleka amesema lengo la ziara hiyo ni kutembelea viwanda vyote vya Wilaya hiyo kwaajili ya kusikiliza na kuzipatia ufumbuzi kero za wa wafanyakazi wa Viwanda hivyo 

Awali akizungumzia shughuli zinazofanyika Kiwandani hapo, Mkurugenzi wa Kiwanda hicho Magaka mponda ameeleza changamoto ambayo wanakumbana nayo kuwa ni uelewa mdogo kwa wananchi kuhusu biashara hiyo ya uvunaji wa utomvu katika mashamba yao.

'' Biashara kwa hapa nchini bado ni mpya hivyo uelewa kwa wananchi bado upo chini wengi wanahofia mitiyao itakufa katika mchakato wa uvunaji lakini tangu wameanza hakuna tatizo lolote ambalo limejitokeza la mti kukauka kutokana na uvunaji wa utomvu huo.'' Alisema Mponda.